Siri katika msamaha

Print Friendly, PDF & Email

Siri katika msamaha

Inaendelea….

Mambo mawili muhimu kwa msamaha; (A) – Toba, Matendo 2:38, Mt. 4:7, Ambayo ni kukiri dhambi na badiliko la mtazamo kuelekea dhambi. Uwe na majuto moyoni kwa ajili ya dhambi zako dhidi ya Mungu: (B) – Ongoka, ambayo ni badiliko katika mwenendo wako, fanya mabadiliko mapya katika mwelekeo na anza mwendo mpya kuelekea kwa Mungu na pamoja Naye.

Zaburi 130:4; Lakini kwako kuna msamaha ili wewe uogopwe.

Matendo 13:38; Basi, na ijulikane kwenu, ndugu zangu, ya kuwa kwa huyo mnahubiriwa msamaha wa dhambi;

Waefeso 1:7; Ambaye katika yeye tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake;

Wakolosai 1:14; Ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, masamaha ya dhambi;

2 Mambo ya Nyakati 7:14; ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.

Zaburi 86:5; Kwa maana wewe, Bwana, u mwema, u tayari kusamehe; na mwingi wa rehema kwa wote wakuitao.

Luka 6:37; Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa; msilaumu, nanyi hamtahukumiwa;

Zaburi 25:18; Tazama mateso yangu na uchungu wangu; na unisamehe dhambi zangu zote.

Mt. 12:31-32; Kwa sababu hiyo nawaambia, Kila dhambi na kufuru watasamehewa wanadamu, lakini kufuru dhidi ya Roho Mtakatifu hawatasamehewa. Na mtu ye yote atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu huu, wala katika ule ujao.

1 Yohana 1:9; Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.

Yeremia 31:34b, “Maana nitausamehe uovu wao, wala sitazikumbuka dhambi zao tena.”

Gombo la 53, Fungu la mwisho; “Adamu aliumbwa na alikuwa amejaa nuru angavu. Alikuwa na karama kwa sababu kupitia kipawa cha maarifa aliweza kuwapa majina wanyama wote. Nguvu ya uumbaji ilikuwa ndani yake wakati mwanamke alipoumbwa (ubavu). Lakini baada ya anguko (dhambi) walipoteza upako mkali na walikuwa uchi wa nguvu za Mungu. Lakini pale Msalabani, Yesu alianzisha mwendo wa kurejesha tena, (kwa njia ya toba na wongofu, ambao ni msamaha). Na mwisho atawarudishia wana wa Mungu kile alichopoteza Adam (mwana wa Mungu). Je, umefika kwenye Msalaba wa Yesu Kristo na umesamehewa? Omba Mungu akusamehe dhambi zako zote kama mwenye dhambi na akuoshe kwa damu yake, katika jina la Yesu Kristo. Yesu Kristo ni Mungu. Kubali tu kwamba Mungu alichukua umbo la mwanadamu na kufa msalabani ili kumwaga damu yake kwa ajili yako. Naye atakuja upesi sana, usichelewe kupata msamaha wako.

059 - Siri ya msamaha - katika PDF